Hosea 9:12-16


12 aHata wakilea watoto,
nitamuua kila mmoja.
Ole wao
nitakapowapiga kisogo!

13 bNimemwona Efraimu, kama Tiro,
aliyeoteshwa mahali pazuri.
Lakini Efraimu wataleta
watoto wao kwa mchinjaji.”


14 cWape, Ee Bwana,
je, utawapa nini?
Wape matumbo ya kuharibu mimba
na matiti yaliyokauka.


15 d“Kwa sababu ya uovu wao wote huko Gilgali,
niliwachukia huko.
Kwa sababu ya matendo yao ya dhambi,
nitawafukuza katika nyumba yangu.
Sitawapenda tena,
viongozi wao wote ni waasi.

16 eEfraimu ameharibiwa,
mzizi wao umenyauka,
hawazai tunda.
Hata kama watazaa watoto,
nitawachinja watoto wao
waliotunzwa vizuri.”

Copyright information for SwhKC